Alhamisi 12 Februari 2026 - 01:30
Umoja wa Ulaya walaani mpango wa kuongeza nguvu ya Israel katika Ukingo wa Magharibi

Hawza/ Umoja wa Ulaya siku ya Jumatatu ulitangaza kulaani uamuzi wa hivi karibuni wa utawala wa Israel wa kuimarisha udhibiti katika Ukingo wa Magharibi.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Umoja wa Ulaya umelaani maamuzi ya hivi karibuni ya Baraza la Usalama la utawala wa Israel yanayolenga kupanua udhibiti wa utawala huo katika Ukingo wa Magharibi.

Anwar Al-Anouni, msemaji wa Tume ya Ulaya, katika mkutano na waandishi wa habari alisema: “Hatua hii ni hatua nyingine katika mwelekeo usio sahihi, wakati ambapo dunia nzima na jumuiya ya kimataifa zinajitahidi kuchukua hatua kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ya mpango wa kina wa Ghaza, Israel inafanya kinyume chake.”

Alibainisha kwamba; uamuzi huo unahatarisha kwa kiwango kikubwa hali nyeti ya maeneo ya ibada.

Al-Anouni pia aliongeza kusema: Kuambatanishwa kwa mujibu wa maazimio ya upande mmoja kwa misingi ya sheria za kimataifa ni kinyume cha sheria; kwa hiyo, hatua yoyote ya vitendo kuelekea lengo hilo itachukuliwa kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Akisisitiza tena kwamba kuchukua hatua dhidi ya ukiukaji wa mara kwa mara wa sheria unaofanywa na Israel bado ni suala lililo mezani, alisema: Tunafuatilia kwa makini maendeleo ya hali halisi uwanjani.

Chanzo: A News

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha